SunFlare Co., Ltd.

Global Interface & Solutions

SunFlare ina rekodi thabiti ya kuwa wakala wa kutegemewa wa ufasiri kwa miaka mingi na inazidi kujituma kuwa mbia wa kiutaalamu mwaminifu kwa wateja wake.
Tunatoa huduma kamili zilizoundwa kwa namna inayotosheleza mahitaji ya kuweka rekodi ya kampuni zinazofanya kazi katika nyanja zote za biashara.
Tuna uwezo wa kuwapa wateja wetu suluhu mwafaka zaidi za kutambua na kushughulikia changamoto zinazohusiana na uwekaji rekodi kwa haraka na kwa usahihi.

Tuna Uthibitisho wa ISO 27001 na ISO 9001

Wateja wetu wana mahitaji mbalimbali ya uwekaji rekodi. Ili kuhakikisha kuwa tuna utaratibu thabiti wa kupokea na kuwasilisha taarifa za kisiri za wateja na kuwa na uwezo wa kutoa kiwango cha juu zaidi cha ubora, tunazingatia mifumo tofauti ya usimamizi ya kimataifa.

Tuna uzoefu wa kuhudumu katika sekta, biashara, na nyanja mbalimbali

Ili kuhakikisha tunasalia kuwa mbia wa biashara wa kutegemewa, wataalamu wetu wa sekta na timu za wataalamu wa nyanjani hufanya kazi pamoja ili kuwapa wateja wetu suluhu mwafaka zaidi kwa changamoto wanazokumbana nazo.

Tuna uwezo wa kutumia lugha 90

Ikiwa kampuni inataka kuendeleza biashara yake kivyake katika kiwango cha kimataifa, basi itahitaji kuwa na ufahamu wa lugha na tamaduni za nchi zote inazolenga kuhudumia. Huu bila shaka hautakuwa mwelekeo mzuri wa kibiashara. Hata hivyo, katika SunFlare, tuna wataalamu wa zaidi ya lugha 90 ambao wanafahamu tamaduni za maeneo ambapo lugha hizo zinatumika. Wanaweza kuwapa wateja wetu usaidizi unaowafaa na kwa muda ufaao ili wafanikiwe kama biashara ya kimataifa. Wataalamu wetu wana uzoefu mkubwa wa ufahamu wa ulingo husika pamoja na ujuzi bora zaidi wa lugha, unaotuwezesha kutoa huduma za ubora wa hali ya juu na kwa upesi kwa hati zinazohitaji kiwango cha juu cha utaalamu, kama vile hati za kisheria, makala ya majarida, na hati zinazohusiana na udhibiti.

Maelezo ya Shirika

Jina la Shirika

SunFlare Co., Ltd.

Lilianzishwa

1 Agosti, 1971

Anwani

Ofisi Kuu iliyoko Tokyo:
Jumba la Shinjuku Hirose., 4-7 Yotsuya, Shinjuku-ku,
Tokyo 160-0004, Japan

Mkurugenzi Mwakilishi

Hiroyuki Sasai

Biashara

Uwekaji Rekodi

 • Ufasiri
 • Ujanibishaji
 • Uandishi (nyanja za kiufundi na kimatibabu)
 • Huduma za ubunifu (uundaji, DTP, tovuti na video)

Utoaji ushauri

 • Utoaji ushauri kuhusu uwekaji rekodi
 • Utafiti (sheria, kanuni, viwango na hataza)
 • Usaidizi wa jinsi ya kuwasilisha na kutuma nyaraka za maombi (hataza, masuala ya udhibiti na vifaa vya kimatibabu)

Elimu na mafunzo

 • Shule ya Mafunzo ya SunFlare
 • Mtihani wa Kuhitimu kwa Mfasiri (TQE)
 • Mafunzo kwa mashirika
 • Warsha (hataza na vifaa vya kimatibabu)

Uthibitisho

ISO 27001, ISO 9001, ISO 17100 na Privacy Mark (JIPDEC)
Mmiliki wa Leseni ya Elimu Soko ya Aina ya II kwa Vifaa vya Kimatibabu

Back to Top